Mshambuliaji wa timu ya Azam FC Didier Kavumbagu (wa kwanza kulia) akiwa na viongozi wa timu hiyo kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Azam FC ni miongoni mwa klabu ambazo tayari zimeshaanza mazoei kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) pamoja na ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2015-2016 ambao utaanza mwezi Agosti mwaka huu.
Kwenye klabu ya Azam FC wachezaji wengi walioanza mazoezi ni wale wa kikosi cha pili wakati wachezaji wa kikosi cha kwanza wakiwa ni wachache. Didier Kavumbagu ni moja ya wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza ambao wamejiunga na kikosi cha Azam kwa ajili ya mazoezi kujiandaa ya Kagame na msimu ujao wa ligi.
Kavumbagu amesema, ameamua kurejea kwenye timu yake mapema kwasababu hiyo ndiyo kazi yake na yeye ni mwajiriwa kama waajiriwa wengine hivyo anatii na kuheshimu taratibu na sheria zilizowekwa na mwajiri wake.
Mbali hayo ameeleza pia jinsi hali ya kisiasa ya nchini kwao (Burundi) ilivyoathiri kiwango cha soka lake hasa kwenye mzunguko wa pili wa ligi iloyomalizika Mei 9 mwaka huu. Kavumbagu amesema ndugu zake wengi wapo Burundi, hapa yupo yeye na familia yake ndogo hivyo vitendo vya vurugu vilivyokuwa vikiendelea nchini Burundi vilikua vinamuumiza kichwa kiasi ambacho alishindwa kuendeleza makali yake ya kupachika mabao kama ilivyokuwa kwenye mzunguko wa kwanza.
Ameongeza kuwa, mabdiliko ya kocha pia yaliyofanywa na timu yake ya Azam yalimuathiri kwa kiasi fulani kwasababu kila mwalimu anakuja na aina yake ya uchezaji na wachezaji anaoona wanafit kwenye mfumo anaoutumia.
Lakini akaahidi kwamba, sasahivi yuko vizuri na watu wategemee mambo mazuri toka kwake kwenye msimu ujao wa 2015-2016 ambapo amejipanga kuisaidia Azam kufika mbali kama yalivyo malengo ya klabu hiyo.
Bofya hapa chini kusikiliza stori nzima ya Kavumbagu akieleza kwanini amewahi kurudi Bongo na mipango yake kwa msimu ujao;
0 comments:
Post a Comment