Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema anashangazwa suala la kocha mpya
wa Simba kuwa gumzo sana na kusisitiza, watu wavute subira.
Hans Poppe amekaririwa
na Salehjembe akisema Simba iko
katika hatua ya mwisho kumalizana na kocha huyo.
“Vuteni subira kidogo, mambo
yanakwenda kwa mpangilio. Si lazima kuwe na haraka kiasi hicho, tutawataarifu
bila ya shida,” alisema.
“Najua mna hamu ya kumjua
lakini ni suala ambalo linahitaji umakini. Najua nilishawaeleza tokea mwanzo
kwamba anatokea Uingereza,” alisema.
Tokea kuondoka kwa Goran
Kopunovic kumekuwa hakuna uhakika Simba inamchukua nani huku suala hilo
likiendelea kuwa siri kubwa.
0 comments:
Post a Comment