Gwiji la
zamani la soka , Diego Maradona ameibuka
na kusema angeweza kuwa makamu wa rais wa shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA
endapo Prince Ali angeshinda urais.
Prince Ali ndiye
alikuwa mpinzani pekee wa Sepp Blatter katika uchaguzi mkuu wa FIFA uliofanyika
majuma kadhaa yaliyopita.
Hata hivyo Blatter alishinda nafasi hiyo ya
juu kabisa ya chombo hicho cha mpira wa miguu duniani, ingawa alijiuzulu siku
kadhaa baadaye.
Maradona
aliyeisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka 1986
anaamini alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo kama
Prince Ali angeshinda.
Hata hivyo
haijathibitika kama Prince Ali atagombea tena mara uchaguzi utakapofanyika
mapema mwakani, lakini uwezekano ni mkubwa kwa raia huyo wa Jordan kugombea.
Blatter
ametangaza kuachia ngazi katika shirikisho hilo la soka duniani kutokana na
kashfa za rushwa zilizolichafua shirikisho na sura nzima ya mpira wa miguu.
Maradona
alikaririwa akiiambia ITV kwamba atalisafisha shirikisho hilo kama akipata
nafasi ya kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa chombo hicho.
0 comments:
Post a Comment