Rushwa yakithiri ndani ya FIFA ambapo mtandao wa BBC umeripoti
kuwa, Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Kandanda duniani FIFA Jack
Warner amekumbwa na kashfa nyingine na uchunguzi dhidi yake kuhusiana na
kupotea kwa fedha ambazo zililengwa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti mwaka 2010.
Warner aliitembelea
nchi hiyo miezi kadhaa baada ya tetemeko hilo a kuchangisha kiasi cha dola mia
saba na elfu 50 kutoka FIFA na shirika la mpira wa miguu la Korea kusini kwa
ajili ya kuijenga upya nchi hiyo.
Lakini hata hivyo,
Wachunguzi wa kashfa hiyo ya rushwa inayoikabili FIFA wanasema fedha hizo
zilihamishwa katika Akaunti inayomilikiwa na Bwana Warner kwa ajili ya matumizi
yake binafsi. Aidha miaka minne baadaye
fedha hizo zilikuwa bado hazijatolewa maelezo na Warner mwenyewe amekana tuhuma
zote zilizotolewa dhidi yake
0 comments:
Post a Comment