Kiungo Lansana Kamara raia wa Sierra Leone anayewania kuichezea Yanga ameumia mazoezini.
Kiungo huyo aliumia kifundo cha mguu katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, leo.
Hali hiyo ilisababisha atolewe nje na kupatiwa matibabu na daktari wa Yanga, Juma Sufiani akisaidiana na Jacob Onyango.
Baada ya hapo, Kamara alipumzishwa huku wenzake wakiendelea na mazoezi.
Kwa hisani ya Salehjembe
0 comments:
Post a Comment