Picha zinazoaminika kuwa jezi mpya za Chelsea kwa msimu wa 2015/2016 zimevuja mtandaoni zikiwa ni nembo ya mdhamini mpya .
Mwezi februari mwaka huu, mabingwa hao wa ligi kuu England walitangaza mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya Japan inayotengeneza matairi, Yokohama Rubber Company ambao wanachukua mikoba ya waliokuwa wadhamini wao Samsung.
Yokohama watakilipa kikosi cha Jose Mourinho paundi milioni 40 kwa mwaka ambapo nembo yao itawekwa sehemu ya kifua ya jezi ya Eden Hazard, John Terry na wenzake.
0 comments:
Post a Comment