Ikiwa
joto linazidi kupanda kuelekea fainal ya Uefa
kati ya Fc Barcelona dhidi ya Juventus fc, mfahamu mpuliza kipyenga
CUNETY CAKIR atakayesimama kati katika dimba la Olympia Stadion hiyo
kesho.
Ana umri wa miaka 38 akiwa
amezaliwa huko Instabul, Uturuki Nov 23, 1976, amechezesha zaidi ya michezo 170,
huku mchezo wake wa kwanza wa Uefa Champions league ulikuwa kati ya Skonto fc vs Sliema Wanderers Julai
2003 kama kamisaa.
Aidha Sept, 29, 2010 alichezesha mchezo wa Uefa Champions League
hatua ya makundi kati ya Rubin_kazan na
FC Barcelona ambapo mchezo uliisha kwa sare ya 0-0. Pia alichezesha mchezo kati
ya Chelsea fc na Spartak Moscow.
Raia huyu wa Uturuk pia atakumbukwa
kwa kumpiga kadi nyekundu John Terry
katika kipindi cha kwanza kwenye nusu fainali ya Uefa champions league kati ya Chelsea fc na fc Barcelona, mchezo
ulioisha kwa sare ya 2-2 na kushuhudia Chelsea fc akitinga fainali na kubeba
kombe ikiwa chini ya Robert Di Mateo.
Katika michezo yote
aliyochezesha dhidi ya Fc Barcelona , mchezo uliisha kwa sare na jamaa huyu pia
atakumbukwa na mashabiki wa Manchester United baada ya kumtoa nje Luis Nani kwenye
mchezo dhidi ya Real Madrid ambao ndio
ulikuwa mchezo wa mwisho wa Uefa Champions league kwa kocha Alex Ferguson.
0 comments:
Post a Comment