Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Sserunkuma aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu wa 2014 akifunga mabao 16 na kuwashawishi Simba kumsajili.'
MSHAMBULIAJI aliyeachwa na Simba, Danny Sserunkuma, amesema yuko huru na bado anasubiri maoni ya wakala wake kabla ya kufanya uamuzi.
Sserunkuma, mchezaji wa zamani wa Gor Mahia, ameachwa na Simba mara tu baada ya kumalizika kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Ikiwa ni siku chache baada ya kutemwa na Simba, mshambuliaji huyo amekiri kuzungumza na viongozi wa Gor Mahia, lakini hajafanya uamuzi wa kujiunga nao.
"Bado sijasaini katika klabu yoyote na mkikumbuka nilivyosema hapo awali, ninaendelea kusubiri maoni ya wakala wangu," Sserunkuma amesema katika moja ya mitandao ya kijamii anayoitumia.
Sserunkuma aliachana na Gor Mahia na kujiunga na Simba baada ya kumalizika kwa msimu wa 2014 wa KPL, akisaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa mara 18 wa Tanzania Bara ambao wameshindwa kuridhishwa na kiwango chake na kuamua kumtema.
0 comments:
Post a Comment