Samata (wa kwanza kulia, waliosimama)
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga TP Mazembe
ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta amekiri kwamba Misri waliwazidi kila kitu
katika kipigo cha 3-0 walichovuna Taifa Stars kwenye mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2017 iliyopigwa jana
mjini Alexandria.
“Pambano lilikuwa gumu, jamaa walituzidi kila kitu, jamaa
walitawala kila kitu, ikabidi wote tuwe na kazi ya kulinda. Mtu anapotawala
mpira unakuwa na kazi nyingi, unakimbia sana uwanjani kuliko anayemiliki mpira.
Kocha atakuwa ameona makosa ya timu na atayarekebisha,
mimi kama mchezaji napewa maagizo na wachezaji wenzangu”. Amesema Samatta.
0 comments:
Post a Comment