Bosi wa Manchester United, Louis van Gaal amegoma kuzungumzia hatima ya baadaye ya golikipa, David De Gea ambaye anahusishwa kujiunga na Real Madrid majira haya ya kiangazi.
De Gea amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na amethibitisha kuanza kufikiria hatima yake hususani kutimkia Madrid.
Ripoti ya gazeti la AS inasema United wanataka dau la Euro milioni 46 kumuachia golikipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid, wakati Marca wao wanasema klabu hiyo ya England itakubali Euro milioni 40.
Akizungumza na Spanish TV, Van Gaal amesema: "Sitaki kuzungumzia ishu hii kupitia vyombo vya habari. Nitazungumza na wakurugenzi wangu, sio vyombo vya habari".
Ripoti zinaeleza kwamba United wanajaribu kubadilishana na Sergio Ramos, lakini vyanzo vya habari vinasema Real Madrid hawako tayari kumhusisha mlinzi huyo wa kati.
0 comments:
Post a Comment