Miamba ya kandanda ya Italia, Inter Milan inaendelea na mkakati wa kutumia kitita cha maana majira ya usajili wa kiangazi mwaka huu.
Wakiwa tayari wamekamilisha usajili wa Geoffrey Kondogbia, Inter wanaongoza mbio za kuinasa saini ya kiungo wa Marseille, Gianelli Imbula.
Roberto Mancini ameendelea kuijenga Inter Milan ambayo haitashiriki michuano ya ulaya msimu ujao.
Leo Jumapili, gazeti la Gazzetta dello Sport, ambalo ni chanzo kizuri cha habari za usajili limeripoti kwamba Inter Milan wapo katika mawasiliano na Chelsea wakihitaji kuwasajili mawinga wake wawili, Mohamed Salah na Juan Cuadrado, ingawa Salah pia anahusishwa kutua Fiorentina.
0 comments:
Post a Comment