BBC imeripoti kuwa huenda Russia na Qatar zikapokonywa uwenyeji wa kombe la dunia 2018
na 2022 iwapo ushahidi wa ufisadi utapatikana dhidi yao.
Afisa
wa FIFA Domenico Scala ameiambia jarida moja la Uswisi, Sonntagszeitung, kuwa
haki ya kuandaa mashindano hayo ya dunia itakuwa katika hatari kubwa iwapo
kutaibuka ushahidi wa kutosha kuwa mataifa hayo mawili yalitoa rushwa.
Hata
hivyo Scala amekanusha kuwa hadi sasa hajapata kuona ushahidi wa aina yeyote
dhidi ya mataifa hayo mawili.
Scala
ambaye ni kiongozi wa kamati ya uhasibu na uchunguzi ameseama kuwa iwapo
ushahidi utatokea kuwa uteuzi wa mataifa hayo mawili haukuwa wa kweli na haki
bila shaka watapokonywa uwenyeji wa mashindano hayo.
Hadi
kufikia leo hakuna ushahidi wa kutosha wa kulazimisha Russia na Qatar
kuchukuliwa hatua kwa tuhuma hizo za rushwa.
0 comments:
Post a Comment