Kocha mkuu wa Azam fc, Stewart Hall
Mkurugenzi wa Fedha na utawala wa Azam FC toka nchini Uingereza pamoja na wasaidizi wa benchi la ufundi watawasili ijumaa hii tayari kuanza kazi Azam FC
Kufuatia mabadliko makubwa ya watendaji na mfumo wake wa uongozi, benchi la ufundi la Azam FC sasa litakuwa chini ya Stewart Hall ambaye yupo jijini Dar es Salaam akisubiri kuwapokea wasaidizi wake ijumaa hii.
Watakaowasili ni pamoja na Muingereza mwenye asili ya Uganda Eli Eribankya ambaye atakuwa Meneja utawala na fedha.
Eribankya atasaidiwa na mwanandinga wa zamani wa Azam FC mtanzania Luckson Kakolaki.
Stewart John Hall ambaye anarejea kwa mara ya tatu kuongoza benchi la ufundi la Azam FC. atasaidiwa na Mganda George Best Nsimbe, huku Mark Philips kutoka uingereza akiajiriwa kuwa kocha wa magolikipa. Hawa wote watawasili ijumaa hii.
0 comments:
Post a Comment