Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015
Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne na vipengele vingine.
Kwa mujibu wa wadhamini wa Ligi kuu Tanzania bara, Vodacom timu nne za juu zitanyakua vitita vifuatavyo;
NAFASI
|
TIMU
|
KIASI CHA FEDHA
|
1.
|
YOUNG AFRICANS
|
MILIONI 80
|
2.
|
AZAM FC
|
MILIONI 40
|
3.
|
SIMBA SC
|
MILIONI 28
|
4.
|
MBEYA CITY FC
|
MILIONI 22
|
0 comments:
Post a Comment