Habari njema kwa mashabiki wa Chelsea: Mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo, Luis Felipe hana mpango wa kuondoka Stamford Bridge kwenda Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu.
Ukurasa wa mbele wa gazeti la Marca leo umeripoti taarifa hiyo kwa headline hii “Dice ‘no’ al Madrid ” (He says “no” to Madrid) yaani amesema haendi Real Madrid.
Kwa wiki kadhaa vyombo vya habari vya England na Hispania vimekuwa vikiripoti kwamba beki huyo raia wa Brazil mwenye miaka 29 hana furaha Chelsea na anataka kurudi Vicente Calderon, hivyo Real Madrid wanajaribu bahati yao.
Chelsea walimsajili Filipe Luis kwa mkataba wa miaka mitatu majira ya kiangazi mwaka jana kutoka Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15.8
Kwasasa Felipe yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kinachojiandaa na michuano ya Copa America itayofanyika Chile.
0 comments:
Post a Comment