Kocha Mkuu wa Misri, Hector Cuper ametamba kuwa kikosi chake kilikuwa na nafasi ya kuitandika Tanzania (Taifa Stars) angalau mabao saba.
Cuper raia wa Argentina amesema walipoteza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza.
“Hilo ndiyo lilikuwa tatizo kubwa sana, niliona wachezaji walikuwa na presha ya juu. Ndio maana tulipokwenda mapumziko nikawaambia watulie". Amesema kocha huyo.
“Hawakuwa na haja ya presha kubwa, niliwashauri kucheza soka kama wanavyocheza lakini wafunge na hilo wakalitekeleza,” alisema.
Misri iliifunga Taifa Stars kwa mabao 3-0 katika mabao yaliyopatikana katika kipindi cha pili tu.
Misri ipo kundi moja na Tanzania, Nigeria na Chad na kocha huyo aliyewahi kuinoa Valencia ya Hispania, amejigamba kuwa Misri ina kikosi kipana zaidi ya timu nyingine katika kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment