Jurgen Klopp anatamani kufundisha ligi kuu England akimaliza mapumziko yake, hii ni kwa mujibu wa wakala wake.
Kocha huyo Mjerumani aliondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu baada ya kukaa miaka saba Bundesliga akiwaongozo kutwaa makombe mawili ya Ligi kuu, Kombe la Ujerumani na alifika fainali ya Uefa Champions league.
Wakala wake, Marc Kosicke amesema mipango ya Klopp kwasasa ni kupumzika kufundisha mpira ili kuchaji kichwa chake, lakini atakaporudi kwenye kazi hiyo anatamani kufundisha timu ya England.
Akingumza na SPOX, Kosicke amesema: "Ligi kuu ya England inavutia sana na hatufikirii tu timu nne za juu kwasababu kuna baadhi ya timu kubwa za chini".
Bila shaka hizi ni taarifa njema kwa klabu za Liverpoool na Manchester City ambazo zimeonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Klopp.
0 comments:
Post a Comment