Monday, June 29, 2015

Wakati timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ikiendelea kujiandaa na mchezo wake wa marejeano na timu ya Uganda ‘The Cranes’ kuwania kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), meneja wa timu hiyo Juma Mgunda ameshindwa kujiunga na timu hiyo kutokana na kutopewa barua ya uthibitisho kutoka shirikisho la kandanda nchini TFF juu ya kibarua chake.
Mgunda amesema, mpaka sasahivi bado hajapokea barua yoyote ile kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuthibitisha uteuzi wa nafasi yake kama meneja wa Stars.
“Nilikuwa nategemea kujiunga na timu lakini kikubwa mpaka sasahivi nasubiri barua ya uthibitisho kutoka TFF ili niende kujiunga na kambi. TFF ni taasisi kubwa kwahiyo nasubiri nipewe barua, kwa kifupi ni kwamba mpaka sasahivi bado sijapata barua”, amesema Mgunda.
“Kinachothibitisha kwamba nimeteuliwa kule ni barua, lakini ‘technical bench’ na wenzangu wengine wameshafika na tayari mazoezi wameshaanza na bahati nzuri ‘program’ ya ‘chief coach’ inaendelea kwahiyo ni matumaini yangu kwamba mimi kuchelewa kufika kambini si kwamba kutakuwa kunazuia kitu kwasababu shughuli zote zinaendelea kama kawaida”, Mgunda amefafanua.
Stars kwa sasa imeweka kambi yake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam (Kiromo, Bagamoyo) ikifanya mazoezi chini ya kocha mpya Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Hemed Morocco.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video