KIUNGO mkongwe na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Henry Joseph Shindika ameonesha nia ya kujiunga
na Mwadui FC wakati huu hana timu yoyote tangu amalize mkataba Mtibwa Sugar msimu uliopia.
Henry aliyewahi kutamba na Simba SC miaka ya nyuma kabla ya
kutimkia Kongsvinger ya Norway, amemalizana na Mtibwa katika msimu uliomalizika
hivi karibuni na yupo huru kutua popote lakini ameanza kwa kuitaja Mwadui
iliyopanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Henry ameiambia Salehjembe kwamba
kikubwa anachovutiwa nacho Mwadui ni kwenda kucheza na wachezaji wazoefu na wakongwe
ambao wapo kwenye kikosi hicho.
“Bado sijajua kama nitaendelea na Mtibwa ama vipi, kwa sababu bado
nawasikilizia lakini hata timu nyingine pia nipo tayari kuzichezea, timu kama
Mwadui ipo poa, katika hizi zilizopanda inaonekana kama iko poa kwenye uongozi
na sehemu nyingine, ndiyo maana wamefika hapa.
“Halafu kitu kingine ina wachezaji wazoefu wa ligi ambao wengi nafahamiana nao,
kwa hiyo nikicheza sehemu kama hiyo haitakuwa taabu sana kucheza mpira mzuri
kwa kuwa wengi mno mnajuana na mnakuwa na morali ya aina moja katika
mapambano,” alisema Henry.
Mwadui iliyo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, imepanda kushiriki ligi
kuu ikiwa na nyota wengi waliowahi kutamba huko nyuma lakini imeongeza pia
wengine.
Baadhi ya wachezaji wao wazoefu ni Shaban Kado, Athuman Idd
‘Chuji’, Uhuru Selemani, David Luhende, Nizar na Razak Khalfan, Jabir Aziz na
Rashid Mandawa.
0 comments:
Post a Comment