Kiungo Mcameroon, Alex Song amerejea Barcelona baada ya kumaliza msimu akikipiga West Ham kwa mkopo na mtu wa kwanza aliyeungana naye alikuwa Neymar Jr.
Neymar ni kati ya washikaji wa karibu wa Song na waliungana pamoja huku wakiwa wamevaa kofia na fulana zinazofanana.
Song, mchezaji wa zamani wa Arsenal amemaliza msimu katika Ligi Kuu England akiitumikia West Ham na amerudi Barca huku akisubiri fainali ya Uefa Champions League watayopigwa juni 6 mwaka huu mjini Berlin.
Hata hivyo hakuna uwezekano wa Song kucheza mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment