“Nilijiskia mkamilifu kwa kugombea tena kwenye uchaguzi wa FIFA nikiamini kwamba kilikua ni kitu muhimu kwa FIFA. Uchaguzi umeisha lakini changamoto za FIFA hazijaisha.
Japokua nina madaraka kutoka kutoka kwa wanachamana wa FIFA, lakini sijiskii kama nina madaraka kutoka kwa dunia nzima ya wapenda soka, wachezaji na vilabu. Pia kwa watu wanaopumua na kupenda mpira na FIFA pia.
Kwa hiyo nimeamua kujiuzulu madaraka yangu niliyopewa na wanachama wa FIFA. Nitaendelea kuwa Rais hadi pale uchaguzi utakapo fanyika. Mkutano wa FIFA utakaofuatia kwenye ratiba ulitakiwa ufanyike 13 May 2016, lakini hiyo italeta ucheleweshwaji usio wa lazima. Nitaiagiza kamati iandae mkutanao mapema kadri inavyowezekana kumpata mrithi wangu”
0 comments:
Post a Comment