BAADA ya jana TFF kutoa maamuzi
kuhusu utata uliojitokeza kwenye mkataba kati ya klabu ya Simba na Ramadhani
Singano ‘Messi’, leo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans
Poppe amesika kwenye kituo kimoja cha redio cha jijini Dar es Salaam akizungumzia
sakata hilo huku akihoji ni nani aliye mwambia Singano yupo huru?
Poppe amesema kikao
kilichofanyika jana na kuongozwa na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa
hakikuwa na mamlaka wala madhumuni ya kuamua upi ni mkataba halali kati ya
mkataba alionao Messi au mkataba uliopo Simba, badala yake kilikuwa ni kikao
cha kutafuta suluhu ili mambo yaweze kwenda sawa kati ya pande hizo mbili.
“Kikao kilichofanyika jana
hakikufanyika kwa madhumuni ya kuamua nani kashinda na nani kashindwa, hakikuwa
na ‘mandate’ hayo, hakina maamuzi ya kusema mkataba huu ni halali na huu sio
halali. Katibu mkuu wa TFF amesema wazi kilichofanyika jana ni ‘mediation’,
pale hapakuwa na maamuzi ya kuchambua mkataba upi upo ‘right’ wala hawakufikia
hatua hiyo”, amesema Poppe.
“Ila walichokisema pale ni
kwamba, kabla hatujafika kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ambako
pale ni mashtaka sasa na hukumu, hivi hili suala halizungumziki? Ndio kitu
kilichofanyika jana na kilitokana na yeye mwenyewe ‘Messi’ kuulizwa, wewe
ulivyozua hili varangati Simba ulikuwa unataka nini, kuondoka Simba?
Akasema hapana mimi nataka kuendelea kuchezea Simba. Akaulizwa mwakilishi wetu
Collins akasema mbona sisi na mkataba tumesha mpatia?”, aliongeza.
“Ndio wakasema kama suala liko
hivi linazungumzika, kwanini lisiende kwenye mkondo huo. Kumbuka mwanzo mimi
nilieleza kuwa, huyu mchezaji wakati amekuja kuhoji kuhusu mkataba wake na
kuona kwamba yeye anazungumzia mkataba wake umeisha na sisi tunasema haujaisha,
tulimweleza kwamba hili suala linazungumzika vizuri tu, kama wewe huutaki huu
mkataba njoo tukae tukupe mkataba mpya lakini mkataba wako ni huu sasa yeye
akaendelea kung’ang’ania na sisi tunaona hili suala ni bora lifike mwisho
wake”, amesema.
“Kama hatutaelewana hakuna
mkataba mpya mezani tunarudi kwenye mkataba wetu ulipo kwamba sisi mkataba wetu
unamalizika 2016, sasa ndio tutakwenda kwenye kamati ya sheria na hadhi za
wachezaji hao ndio watakaotoa uamuzi sasa mkataba upi ni halali”, amefafanua.
“Baada ya kutoka kwenye kikao
cha jana, Messi kaenda kuzunmgumza kwamba yeye yuko huru sasahivi, aliyemwambia
yuko huru nani? Mwesigwa kaulizwa pale kama mchezaji yupo huru kasema hapana,
na haikutakiwa kuzungumza, mtu aliyetakiwa kuzungumza pale alikuwa ni katibu
peke yake”, alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment