Cristiano Ronaldo ameiambia Real Madrid kwamba ataendelea kuwepo klabuni hapo msimu ujao baada ya Rafa Benitez kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Santiago Bernabeu.
Benitez tangu kuteuliwa kwake wiki mbili zilizopita amekuwa akiongea na wachezaji muhimu wa klabu hiyo na tayari amezungumza na Ronaldo aliyeifungia Ureno 'Hat-trick' jana usiku ikishinda 3-2 dhidi ya Armenia kufuzu Euro 2017.
Mshambuliaji huyo amemhakikishia Benitez kubaki Bernabeu licha ya Paris Saint-Germain kumhitaji.
Pia Ronaldo hana mahusiano mazuri na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez na hii ilikuwa moja ya sababu ya nyota huyo kutaka kuondoka zake.
Mkataba wa Ronaldo Bernebeu unamalizika mwaka 2018 na inafahamika kwamba anavuna paundi milioni 14 kwa mwaka.
Mbali na kuzungumza na Ronaldo, Benitez alikutana na Gareth Bale juzi huko Cardiff ambapo timu ya taifa ya Wales ilishinda 1-0 dhidi ya Ubelgiji kuwania kufuzu Euro 2016.
Kocha huyo aliyeanzia kazi Bernabeu miaka 20 iliyopita alimtaka Bale kujua kwamba bado ana umuhimu mkubwa Real na atarudisha makali yake wakati wa maandalizi ya kabla ya msimu (Pre-season).
0 comments:
Post a Comment