TAARIFA za usajili za hivi punde zinaeleza kwamba mmliki wa Tottenham, Daniel Levy amemhakikishia kocha mkuu wa klabu hiyo, Mauricio Pochettino kwamba hatamuuza mshambuliaji, Harry Kane au Hugo Lloris katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.
Hili ni pigo kwa Manchester United ambao wanajipanga kutuma ofa Spurs wakihitaji saini ya Kane ili kuziba pengo la Radamel Falcao ambaye amerudishwa katika klabu yake ya Monaco baada ya kushindwa kuonesha cheche chini ya Louis van Gaal.
Wakati huo huo Robin van Persie naye hana uhakika wa kuendelea kuwepo Old Trafford..
0 comments:
Post a Comment