Klabu ya Ac Milan imethibitisha kumtimua kocha wake, Filippo Inzaghi baada ya kuwa na
msimu mbaya katika ligi ya Serie A na nafasi yake inachukuliwa na Sinisa
Mihajlovic.
Mihajlovic ambaye
alikuwa kocha wa Sampdoria msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka miwili
kukinoa kikosi hicho na atalipwa karibia paundi milioni 2.5 kwa msimu.
Licha ya kumtimua kocha
huyo AC Milan wamempongeza kwa kazi yake aliyoifanya akiwa kwenye klabu hiyo.
Ac Milan chini ya
Inzaghi imemaliza msimu uliopita ikiwa
imeshika nafasi ya kumi ikijikusanyia
52, wakati Mrithi wake Sinisa alimaliza nafasy ya 7 akiwa na Sampdoria.
0 comments:
Post a Comment