Timu ya taifa ya wanawake ya England imefuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga wenyeji wa michuano hiyo timu ya Canada kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo.
Magoli yote mawili ya England yalifungwa kipindi cha kwanza na Jodie Taylor pamoja na Lucy Bronze yameipeleka England kwenye hatua ya nusu fainali ambako itakutana na Japan ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo kwenye mchezo utakaopigwa siku ya Jumatano ijayo.
Christine Sinclair alifunga goli pekee la kufutia machozi kwa upande wa wenyeji Canada akitumia makosa ya Karen Bardsley.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa England kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwenye historia ya soka la wanawake nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment