Friday, June 5, 2015

Na Ramadhani Ngoda.
Mchezaji wa Tennis namba moja kwa ubora ulimwenguni kwa upande wa wanaume Mserbia Novack Djokovic leo anatarajiwa kuvaana na Muingereza Andy Murray katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa.

Djokovic ambaye alimuondosha Mhispania Rafael Nadal katika mchezo wa robo fainali kwa seti 7-5 6-3 6-1 na kuandika kipigo cha pili kwa Nadal katika michezo yake 8 ya hivi karibuni, anaingia katika mchezo huo huku rekodi ikionesha kuwa ameshamchapa Muingereza huyo mara 18 dhidi ya mara 8 tu alizowahi kushinda Murray kwa mbabe huyo.

Kingine cha kujivunia kwa Mserbia huyo ni kushinda michezo yote 7 iliyopita dhidi ya Murray huku mchezo pekee wa mwisho Murray kumshinda Djokovic ni fainali ya Wimbledon nyumbani kwao mwaka 2013.


Andy Murray aliyemuondosha Dvid Ferrer katika mchezo wa robo fainali kwa seti 7-6 (7-4) 6-2 5-7 6-1, anaingia katika nusu fainali hiyo akiwa na kumbukumbu ya kipigo cha seti 4 alichokipata katika fainali ya michuano ya wazi ya Australi dhidi ya Djokovic mapema mwaka huu hivyo inabidi afanye kazi ya ziada kubadili kinachoonekana kuwa unyonge akutanapo na kinara huyo wa dunia kwa sasa.

Djokovic hakusita kuutambua uwezo wa Murray na kukubali kuwa utakuwa mchezo mgumu kwake licha yay eye kuwa namba moja kwa ubora.

“Ni mchezaji aliye juu kwa sasa, hakuna shaka juu ya hilo. Amekuwa akicheza mchezo mzuri sana,” alisema Djokovic

Kwa upande wake Murray ameapa kufanya awezalo ili kuandika kipigo cha pili kwa Mserbia huyo ndani ya mwaka huu.

“Inategemea na jinsi ulivyojiandaa kuelekea mchezo wenyewe. Nitafanya ambacho nimekuwa nafanya kushinda mchezo,” alijigamba Murray.

Atakaeshinda katika mchezo huo atavaana mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga aliyetinga nusu fainali kwa kumchapa Mjapan Kei Nishikori dhidi ya Mswis Stan Wowrinka aliyemuondosha Mswis mwenzake Rodger Ferderer katika mchezo wa robo fainali.

Kama Tsonga atamshinda Wowrinka na kutinga fainali itakayopigwa siku ya jumapili kisha kutwaa taji hilo, atakuwa ameweka rekodi ya Mfaransa wa kwanza kutwaa taji hilo la ‘French Open’ katika ardhi ya nyumbani tangu Yannick Noah alipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1983.






0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video