kufuatia tetesi za wiki kadhaa, Gazeti la Jumapili la Telegraph limebeba stori kubwa ya usajili (tazama ukurasa wa nyuma chini) ambayo inasema dili la Radamel Falcao kutua Chelsea kwa 90% limekamilika.
Imeelezwa kwamba mshahara wa Falcao wa paundi 265,000 kwa wiki utapunguzwa, kimethibitisha chanzo kilicho karibu na klabu ya Chelsea.
Kwa mara nyingine tena Falcao anatolewa kwa mkopo kutoka Monaco kwenda Chelsea kwani msimu uliopita aliichezea Manchester United iliyogoma kumnunua kwa dau la paundi milioni 43 kutokana na kushindwa kuonesha cheche.
Wakala wa Falcao, Jorge Mendes yuko karibu mno na Jose Mourinho kuhakikisha dili linakwenda sawa.
Likikamilika Mcolombia huyo atacheza timu moja na mchezaji mwenzake wa zamani wa Atletico Madrid, Diego Costa.
Cha kushangaza Chelsea imeamua kumtoa Loic Remy ambaye aliifungia The Blues baadhi ya magoli muhimu msimu uliopita na tayari klabu za Crystal Palace na West Ham zimevutiwa na mshambuliaji huyo.
Kama Alan Pardew atamshawishi Remy na Yohan Cabaye akaungana naye, halafu akafanikiwa kumbakisha Yannick Bolasie, tai hao watakuwa na safu kali ya ushambuliaji.
0 comments:
Post a Comment