Micho |
UKIMSIKILIZA kocha wa timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’,
Milutin Micho unagundua kirahisi kwamba hana wasiwasi kuwavaa Tanzania katika
mechi ya kesho ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa
ndani CHAN.
Akizungumza jioni hii mjini Zanzibar, Micho amesema mechi ya
kesho ni kama maandalizi ya mipango yake ya baadaye, ingawa anawaheshimu
Tanzania.
“Nina malengo yangu nimejiwekea, tumetoka kuwafunga 2-0
Botswana kuwania kufuzu Afcon 2017. Kesho tunacheza na Tanzania, siwadharau
Tanzania, lakini mechi ya kesho nitaitumia kama sehemu ya maandalizi ya mipango
yangu mingine. Najua tutafanya vizuri”. Amesema Micho.
Usiku wa leo kuanzia majira ya saa mbili, Uganda watafanya
mazoezi katika uwanja wa Amaan Zanzibar utakaotumika katika mechi ya kesho.
0 comments:
Post a Comment