SIMBA imeamua kufanya mambo yake kimyakimya na kufanikiwa
kunasa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
Habari za uhakika zimeeleza, Simba
imemsajili Mavugo kwa mkataba wa miaka miwili na mjumbe wa kamati ya utendaji,
Collins Frisch ndiye alifanya kazi hiyo mjini Bujumbura, wiki iliyopita.
“Kweli alikuja hapa yule ofisa wa Simba, wamemalizana na
Mavugo na kila kitu kimekwenda sawa,” Chanzo kutoka Bujumbura kimekaririwa na Salehjembe.
Hata hivyo imekuwa ikielezwa kwamba Mavugo ana mkataba
binafsi na bosi wa timu yake ya Vital'O jambo ambalo Simba lazima walimalize
kabla ya kupata uhamisho.
Simba ilikuwa ikishindwa kufanikisha dili hilo kwa straika
huyo aliyekuwa akikipiga katika timu ya Vital’O baada ya kuibuka kwa machafuko
ya kisiasa yaliyoenea nchini Burundi kutokana na baadhi ya raia wa nchi hiyo
kupinga kitendo cha Rais Pierre Nkurunziza kuwania nafasi hiyo kwa awamu ya
nne.
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba,
Collin Frisch alitinga Burundi kwa ajili ya kwenda kujua mbivu na mbichi juu ya
hatma ya kumtia mikononi mchezaji huyo na hatimaye akarejea na jibu zuri.
Mavugo aliyewahi kuzitumikia
Polisi ya Rwanda na SC Kiyovu anatua Simba akiondoka na rekodi nzuri nchini
Burundi baada ya kuisaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Burundi
msimu wa 2014/15.
0 comments:
Post a Comment