Sunday, June 28, 2015

Mchezaji anae shikilia tuzo ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo amevunja ukimya uliokuwepo kwa muda mrefu baada ya kufunguka juu ya taarifa za vyombo vya habari zinazoripoti kuwa hana furaha kwenye klabu ya Real Madrid na huenda anatafuta mlango wa kutimkia kwenye klabu hiyo.
Ronaldo amenukuliwa na gazeti moja la michezo la nchini Ureno linalofahamika kwa jina la A Bola la Jumamosi akisema kwamba, anafuraha kuwa kwenye klabu bora duniani, anajipanga  na anahakika msimu ujao utakuwa ni wa mafanikio.
Ronaldo 2“Taarifa kwamba nitaka kusababisha mfarakano baina yangu na Real Madrid hazina ukweli wowote”, Ronaldo alinukuliwa na gazeti hilo.
“Nina furaha sana kuwa kwenye klabu bora duniani, ninajipanga na ninaimani msimu ujao utakuwa ni wa mafanikio”, aliliambia gazeti hilo.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno amezungumza hadharani tangu alipowaambia waandishi wa habari kwamba, hatozungumza kwenye vyombo vya habari hadi mwisho wa msimu baada ya timu yake kupata kichapo kwenye mechi ya vilabu bingwa barani Ulaya kutoka kwa Schalke 04 mwezi Machi.
Ronaldo 3Licha ya Ronaldo kutupia kambani idadi kubwa ya mabao, Real Madrid ilishuhudiwa ikimaliza msimu mzima bila taji lolote na kupelekea kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Rafa Benitez.
Ronaldo kwa sasa yupo mapumzikoni (likizo) Miami akila maisha baada ya pilika nyingi za msimu uliopita kutokuwa na mafanikio kwa klabu ya Madrid.
Ronaldo 1

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video