Goli pekee la Jose Salomon Rondon katika dakika ya 60' limetosha kuipa ushindi wa goli 1-0 timu dhaifu ya Venezuela dhidi ya Colombia katika mechi ya ufunguzi ya kundi C ya kombe la mataifa ya America kusini (Copa America).
Radamel Falcao alikuwa anatazamwa na mashabiki wa Chelsea pamoja na kocha Jose Mourinho ambaye anakaribia kumsajili kwa mkopo kutoka Monaco, lakini kiwango alichoonesha jana kinaweza kuzua maswali.
Ingawa Falcao alijitahidi kukaa na mpira, hakuwa na jipya mbele ya walinzi wa Venezuela.
Tangu kupata majeraha ya goti mwaka juzi, Falcao hajarudi kwenye kiwango chake, lakini Mourinho anasema nyota huyo mwenye miaka 29 bado anaweza kuwa na cheche licha ya kukumbuwa na ukame wa magoli.
0 comments:
Post a Comment