Tuesday, June 16, 2015

Timu ya taifa ya Chile imelazimishwa sare ya 3-3 na timu ya taifa ya Mexico katika mechi ya pili ya kundi A ya michuano ya mataifa ya America kusini (Copa America) iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.
Mexico walikuwa wa kwanza kuandika goli la kuongoza dakika ya 21' kupitia kwa Matias Vuoso, lakini dakika moja baadaye Arturo Vidal akasawazisha.
Dakika ya 29' Raul Jimenez akaiandikia Mexico goli la pili ambalo lilisawazishwa na Eduardo Vargas dakika ya 42'.
Arturo Vidal soars above the Mexico defence to equalise for Chile shortly after Vuoso's opening goal
Ngoma iliendelea kuwaka moto ambapo dakika ya 55' kiungo wa Juventus, Arturo Vidal kwa mara ya pili aliifungia Chile goli la tatu, lakini halikudumu sana kwani dakika ya 66' Matias Vuoso alifuta goli hilo na kuufanya ubao usomeke 3-3 mpaka dakika 90' zinamalizika.
Mechi nyingine ya kundi hilo Bolivia imeichakaza 3-2 timu ya taifa ya Ecuador.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video