Thursday, June 18, 2015

MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United,Abasalim Chidiebele amesaini kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Chidiebele alitua mkoani Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliano na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo utiaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai na viongozi wengine.
Akizungumza mara baada ya kusaini,Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuahidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.
  “Nashukuru kusajili Coastal Union kikubwa ninawaahidi tu wapenzi,wanachama na mashabiki kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu", alisema Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini.
Kwa upande wake,afisa habari wa klabu ya Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaoweza kuwahakikisha ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara.
   “Unajua usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao", alisema.
Hata hivyo aliwataka wapenzi na mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video