Chelsea wanajiandaa kutuma ofa ya paundi milioni 30 kwa Straika wa zamani wa Real Madrid, Gonzalo Higuain.
Gazeti la The Sun limeripoti kwamba kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ametia baraka zake kumnunua mshambuliaji huyo raia wa Argentina ambaye ameifungia Napoli inayocheza Seria A magoli 19 msimu uliopita.
Inafahamika kwamba klabu hiyo ya Magharibi mwa London inapambana kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kutokana na Gwiji wa klabu, Didier Drogba kuondoka Stamford Bridge majira ya kiangazi mwaka huu.
Kwa miaka michache iliyopita, Gonzalo Higuain amekuwa akihusishwa sana kujiunga na Arsenal, lakini dili halijawahi kukamilika.
Chelsea pia inahusishwa na kumsajili Mcolombia, Radamel Falcao baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo Manchester United.
0 comments:
Post a Comment