Cannavaro
NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Nadri Haroub ‘Cannavaro’
yupo hatarini kuikosa mechi ya kesho dhidi ya Uganda kuwania kufuzu fainali za
mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN, zitakazofanyika mwakani nchini
Rwanda.
Kocha msaidizi wa Stars, Salum Mayanga amethibitisha kwamba
Cannavaro ni majeruhi, lakini taarifa ya daktari inasema kwamba anaweza kuwa
fiti kufikia siku ya kesho.
“Kutokana na taarifa ya Daktari, Cannavaro anaendelea
vizuri, ni matarajio yetu baada ya mazoezi ya leo jioni atakuwa fiti, hatuna
wasiwasi na hilo, kama lolote litatokea tuna vijana wanaoweza kuziba nafasi
yake na tukafanya vizuri katika mechi ya kesho”. Amesema Mayanga.
0 comments:
Post a Comment