Wednesday, June 3, 2015

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amelishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzindua jezi mpya zitakazotumiwa na Stars kwenye michezo yake ya nymbani, ugenini na mazoezini. Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Golden Jubilee Towers ambapo TFF ilikua inasherekea miaka 50 tangu kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa miguu duniani (FIFA). 
Cannavaro amesema jezi hizo zilizo zinduliwa leo na mgeni rasmi Said Matanda ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya huduma za jamii hazitakuwa urembo bali zitawaongezea chachu ya kufanya vizuri kwenye mechi zao.
“ Kwa niaba ya wachezaji wenzangu, nawashukuru sana TFF kwa kutuletea jezi mpya, jezi hizi hazitakuwa urembo wala hazitatumika kufanyia maonyesho uwanjani, bali jezi hizi zitaongeza chachu ya ushindi kwenye timu ya Taifa. Nawaahidi timu yetu itafanya vizuri kwenye michuano tuliyonayo mbele yetu kikubwa tuzidi kushirikiana ili kuleta mafanikio ya soka nchini” amesema Cannavaro.
Kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa zamani wa FAT na TFF pamoja na wadau wa soka waliochangia maendeleo ya soka Tanzania, baadhi yao walipewa vyeti vya heshima kutokana na TFF kutambua mchango wao kwenye maendeleo ya soka la Tanzania.
Mgeni rasmi katika hotuba yake amesema kuwa, soka la Tanzania limekuwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo wachezaji walikuwa wakicheza mpira bure. Lakini akasisitiza bado halijafikia kiwago kinachotakiwa ukilinganisha na nchi nyingine hivyo zinahitajika juhudi za makusudi kuendelea kupambana kulisogeza mbele ili kuendana na nchi nyingine.
Mtanda ametoa wito kwa TFF kutoa nafasi kwa makocha wazawa ili wapate nafasi ya kuifundisha timu ya Taifa kuliko kuendelea kung’ang’ania makocha wakigeni ambao wanakuja na kuondoka lakini soka letu limeendelea kubaki palepele licha ya makocha hao kulipwa mamilioni ya shilingi na serikali ukilinganiha na mafanikio yanayopatikana.
Tarehe 8 Agosti 1964 Tanzania ilipata uanachama wa kwenye shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, hivyo TFF iliandaa sherehe fupi ya kuadhimisha miaka 50 tangu ianze kutambuliwa kama mwanachama wa FIFA.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video