Monday, June 29, 2015


Uganda vs Tanzania – 4th July 2015 Nakivubo Stadium, 4: 00 p.m"
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) imeteua marefa kutoka Djibouti kwa ajili ya mechi ya Uganda 'Cranes' na Taifa Stars kuwania kufuzu fainali zijazo za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Mechi hiyo itachezwa Jumamosi Julai 4, 2015 kwenye uwanja wa kivita wa Nakivubo ikiwa ni ombi la Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) baada ya uongozi wa Uwanja wa Namboole kutaka ulipwe mpunga mkubwa wa fedha za Uganda (Ush. milioni 40).

Aden Abdi Aden Djamal, atakuwa refa wa kati akisaidiwa na raia wenzake wa Djibout, Abdillahi Mahamoud Il Tireh na Hamze Abdi Salime.
Souleiman Ahmed Djamal, ambaye pia ni raia wa Djibouti, atakuwa mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Osama Ata Elmanan Hassan kutoka Sudan.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video