Tuesday, June 30, 2015

Amependekezwa na Rodgers

Sean O'Driscoll yuko tayari kuachia nafasi yake ya ukocha wa timu ya Taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 19 na kujiunga na benchi la ufundi la Liverpool.

Bosi wa Majogoo, Brendan Rodgers amempendekeza Sean kuwa msaidizi wake namba moja.

Kwa muda mrefu sasa, Liverpool wamekuwa wakitafuta kocha wa kumrithi Colin Pascoe na Mike Marsh ambao wamefukuzwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo msimu uliopita.
Kocha wa kikosi cha vijana chini ya miaka 16 cha Liverpool ,  Pepijn Lijnders amepandishwa timu ya kwanza, huku  O’Driscoll  akitarajia kuungana naye.
Kwa mujibu wa Rodgers, O’Driscoll ndiye kocha bora nchini England na  amewahi kuzifundisha vizuri timu za Doncaster Rovers, Crawley Town, Nottingham Forest na Bristol City.

O'Driscoll alijiunga na FA mwezi septemba kwa ajili ya kufundisha timu za vijana. 
Wakati huo huo,  Mike Marsh  ameripotiwa kuwa na mpango wa kujiunga na Sheffield kesho Jumatano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video