Na Ramadhani ngoda.
Wagonga nyundo wa jiji la London, klabu ya West
Ham United wamethibitisha Slaven Bilic kama kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya
makubaliano ya kusaini mkataba wa maka mitatu.
Mcroatia huyo ametwaa kibarua hicho kwa kumpiga
chini Marcelo Bielsa aliyekuwa akiwania naye nafasi hiyo iliyoachwa na kocha
aliyetimka klabuni hapo Sam Aladyce ‘Big Sam’
Bilic hakusita kuonesha furaha yake kurejea katika
klabu aliyoichezea kwa miezi 18 tu mwaka 1996 na 1997.
“Nimefurahi kurudi West Ham United. Naikumbuka
West Ham kama klabu ya kipekee sana. Nawapenda vijana wa klabu hii ya kipekee,”
alisema Bilic.
“Kigezo change kikuu ninapochagua timu huwa
nimalengo ya timu. Malengo na ari ya West Ham ipo katika kuwa klabu kubwa. Hiyo
ni moja ya sababu kubwa iliyofanya nione kweli wananihitaji,” alisitiza
Mcroatia huyo.
West Ham waliomaliza nafasi ya 12 katika msimu wa
ligi uliomalizika wakivuna point 47, sawa na Everton na moja nyuma ya Crystal
Palace waliomaliza wa 10, wapo katika harakati za kujenga kikosi kwa kuongeza
baadhi ya wachezaji akiwemo kiungo Pedro Biang wa Sampdoria.
Licha ya kuongeza wanandinga wapya katika klabu
hiyo, bado Bilic atakuiwa na kibarua cha kubakisha wachezaji waliotia nia
kutimka Upton Park akiwemo mshambuliaji Carlton Cole.
0 comments:
Post a Comment