Monday, June 29, 2015

Nathaniel Clyne anajiandaa kwenda kuchukua vipimo vya afya katika klabu ya Liverpool leo kabla ya kukamilisha usajili wake kutokea klabu ya Suouthampton.
Clyne, 24, anatarajia kusaini mkataba wa miaka mitano kufuatia timu zote mbili kukubaliana dili hilo wiki iliyopita.
Awali Liverpool waliweka mezani paundi milioni 10 ambazo zilikataliwa mwezi Mei mwaka huu, lakini waliboresha dau mpaka kufikia paundi milioni 12.5 ambazo Southampton wamekubali.
Mlinzi huyo wa pembeni wa England, ambaye ameichezea timu ya Taifa mechi nne anakaribia kukamisha taratibu zote za kutua Merseyside.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video