Hatimaye yamekuwa, Dani
Alves amesaini mkataba wa miaka miwili na timu yake kongwe ya Barcelona.
Alves mwenye umri wa
miaka 32, raia wa Brazili, alihusishwa na tetesi nyingi za kuihama klabu yake,
huku Mashetani wekundu kuonekana kuiwinda sana saini yake.
“FC Barcelona
imetangaza kuwa Alves amekubal ombi la klabu hiyo ya kutaka kuendelea
kuichezea”, mtandao wa Blaugrana umeripoti.
Beki huyo wa kulia wa
Barcelona alionesha jitihada kubwa na
kusaidia klabu yake kutwaa makombe matatu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment