Kocha wa FC Barcelona, Luis Enrique ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwafundisha mabingwa hao wa Ulaya.
Kiungo huyo wa zamani wa Barca na Real Madrid amefikia makubaliano katika mkataba ambao utamuweka Nou Camp mpaka mwaka 2017.
Enrique amefurahia mafanikio Barca akitwaa kombe la La Liga, Copa del Rey na mwishoni mwa juma alishinda Uefa Champions League akiifunga 3-1 Juventus kwenye mechi ya fainali iliyochezwa Olympiastadion, Mjini Berlin, Ujerumani.
"Tumekubaliana kumuongeza Luis Enrique mkataba mpaka mwaka 2017, kwahiyo tutakuwa na Luis Enrique kwa miaka miwili zaidi," Amesema Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu
0 comments:
Post a Comment