Na Ramadhani Ngoda.
Mabingwa
wapya wa Ulaya klabu ya FC Barcelona inajiandaa kumtangaza kiungo wa pembeni wa
FC Sevilla, Aleix Vidal kama ingizo jipya katika klabu hiyo baada ya
kukamilisha usajili wake siku ya jumamaosi.
Licha
ya kuwa katika kifungo cha kutosajili mpaka mwaka 2016, mabingwa hao wa
Hispania na Ulaya wamekuwa katika harakati za kunasa saini kadha wakadha kwa
ajili ya kuboresha kikosi chao ingawa watatakiwa kusubiri hadi Januari 2016 ili
kuanza kuwatumia wachezaji hao.
Aleix
Vidal amesaini mkataba wa miaka 5 na Barcelona siku ya Jumamosi baada ya klabu
hizo mbili kukubaliana juu ya ada ya uhamisho inayotajwa kufikia pauni milioni
10.
Winga
huyo anayeweza kucheza pia nafasi ya mlinzi wa pembeni, anatarajiwa kuwa nyongeza
na mbadala sahihi wa beki wa Kibrazil Dani Alves ambaye licha ya juhudi za
raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu kumbakisha Camp Nou, anaonekana
kuikaribia milango ya Old Trafford na kufata nyayo za Victor Valdes aliyejiunga
na mashetani wekundu hao msimu uliomalizika.
Mhispania
huyo aliyesajiliwa na Sevilla msimu uliopita akitokea Almeria alikocheza
michezo 120 na kufanikiwa kupachika wavuni mabao 17, ameichezea Sevilla michezo
31 msimu huu na kufumania nyavu mara 4 huku akitengeneza mabao 11 na kuisaidia
vilivyo Sevilla katika mafanikio yake ya kombe la Europa msimu huu.
Sasa
Vidal atatambulishwa rasmi siku ya jumatatu kwenye mkutano maalumu na waandishi
wa habari kama mchezaji halali wa wafalme hao wa bara la Ulaya baada ya kufaulu
vipimo vya afya.
0 comments:
Post a Comment