Chelsea wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo, Radamel Falcao, hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa soko la usajili, Gianluca Di Marzio.com.
Kwasasa Mcolombia huyo yupo katika majukumu ya timu ya taifa inayoshiriki michuano ya Copa America na ameonesha nia ya kuendelea kubaki England, licha ya kufanya vibaya akiwa na Manchester United.
Falcao alicheza msimu uliopita Man United kwa mkopo akitokea klabu ya Monaco, lakini baada ya kushindwa kumshawishi Louis van Gaal, United wameamua kuachana na mpango wa kumnunua, hivyo amelazimika kurudi Monaco.
Klabu yake pia haipo katika mazingira ya kumhitaji kutokana na gharama kubwa anazohitaji na wanaweza kumuuza majira ya kiangazi, ila Chelsea wanahitaji kumchukua kwa muda mfupi.
0 comments:
Post a Comment