Kiungo kutoka nchini Ubelgiji, Marouane Fellaini ameupinga ujumbe ulioandikwa katika akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, kumuhusu mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina Angel di Maria.
Kiungo huyo wa klabu ya Man Utd, ameshutumiwa kuandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri Di Maria katika maisha yake mapya atakapokua na klabu bingwa nchini Ufaransa Paris St Germain *PSG* msimu ujao wa ligi, kwa kuamini ni mchezaji mwenye hadhi kubwa duniani.
Kituo cha televisheni cha nchini Ufaransa *Telefoot* kiliuonyesha ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Fellaini kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambao ulisomeka “Angel di Maria atakuwa chaguo sahihi kwa mabingwa wa nchini Ufaransa PSG endapo atasajiliwa na klabu hiyo:
Fellaini amesema hakuandika ujumbe huo katika mtandao wa Twitter na anahisi mbinu zinazofanywa kwa sasa ni kutaka kumgombanisha na baadhi ya viongozi huko Old Trafford ambao watakua wamekasirishwa na ripoti hiyo iliyotolewa na kituo cha televisheni cha nchini Ufaransa.
Pia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amedai kutengezenewa mazingira mabaya dhidi ya mchezaji mwenzake Angel di Maria, ambapo anaamini atakua hakupendezwa na taarifa hiyo.
Angel di Maria amekua katika minong’ono ya muda mrefu ya kuwa mbioni kuondoka Old Trafford, baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake tangu aliposajiliwa na Man Utd mwanzoni mwa msimu wa 2014-15.
0 comments:
Post a Comment