UONGOZI wa klabu ya Azam FC upo katika hatua ya mwisho kumnasa kiungo wa kimataifa wa APR ya Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza, ili kuwadhibiti washambuliaji machachari wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwamo Warundi Amissi Tambwe na Laudit Mavugo, anayewaniwa na Simba na wengineo.
Tayari mazungumzo baina ya mchezaji huyo na Azam FC yamefikia pazuri na kwamba kilichobaki ni kusaini mkataba wa kukitumikia kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mugiraneza amekubali kujiunga na Azam FC baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Kagame, ambayo imepangwa kufanyika mwezi Julai, jijini Dar es Salaam, ambapo El Marreikh ya Sudan ndio mabingwa watetezi.
Endapo Mugiraneza atafanikiwa kujiunga na kikosi cha Azam, ataimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo msimu uliopita ilikuwa chini ya Nahodha Agrey Morris, Paschal Wawa, Erasto Nyoni, Said Mourad na kuifanya ngome ya timu hiyo kuwa tishio kwa washambuliaji machachari kama Amis Tambwe na Laudit Mavugo, anayewaniwa na Simba.
Chanzo:Bingwa.
0 comments:
Post a Comment