SIKU moja baada ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Ramadhan Singano 'Messi' kuonekana katika viungo vya makao makuu ya Azam fc eneo la Mzizima jijini Dar es salaam, uongozi wa klabu hiyo umekanusha kumsainisha nyota huyo.
Taarifa zimesambaa kwenye vyombo vya habari kwamba Azam imemsajili Messi ambaye ana mgogoro wa kimkataba na klabu yake ya Simba, lakini makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Nassor Idrissa 'Father' amekanusha habari hizo akidai hawajaingia kandarasi yoyote na Messi.
"Ramadhan Singano sina hakika nalo kwasababu mimi sikumuona kwa macho yangu, hata kama kuna mtu alimuona sio tatizo, ofsi zetu si jela au mahakama, Singano ni mtu huru,anaweza kuonekana si tatizo". Amesema Idrissa na kufafanua: "Hakuna kandarasi yoyote tuliyoingia na Messi, hatujazungumza naye, narudia maneno yangu, kwa macho yangu sikumuona katika ofsi zetu"
Hata hivyo Azam wanaiwinda saini ya Messi na kama sakata la mkataba wake litakwisha, wanaweza kumsainisha wakati wowote.
Messi anadai alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu yake ya Simba Mei 1, 2013 na unamalizika Julai 1, 2015, wakati Simba wao wanasema alisaini mkataba wa miaka mitatu Mei 1, 2013 na utakwisha Julai 1, 2016.
0 comments:
Post a Comment