MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc
wameanza mazoezi rasmi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2015/2016 baada ya
makocha wote kuwasili nchini.
Afisa Mtendaji mkuu wa Azam, Saady Kawemba ameuthibitishia
mtandao huu kwamba wataalamu wao waliwasili Ijumaa iliyopita, Jumamosi
wakafanya kikao na utawala na wakapata fursa ya kutembelea Uwanja wa Azam
Complex kuona miundombinu iliyopo na jana wamewatambulisha rasmi kwa wachezaji.
“Wachezaji wamewatambua viongozi na makocha wao, kwakweli makocha
wamekuwa na furaha kujiunga na timu hii na leo tumeanza rasmi mazoezi kuanzia
saa mbili na nusu asubuhi”. Amesema Kawemba na kuongeza: “Kwasasa wachezaji wa
timu ya wakubwa na wadogo wanafanya mazoezi pamoja kwasababu wachezaji 14 hawapo,
wapo kwenye timu zao za taifa, watakaporejea tutaanza mazoezi ya kila timu
kujitegemea”
Kawemba pia amegusia programu ya kocha, Stewart John Hall aliyerejea kwa mara ya tatu kuifundisha Azam.
“Kutokana na kikao cha jana, Mwalimu (Stewart) amesema kwa wiki nzima hii
atatengeneza akili za wachezaji, kwamba
sasa tunaanza msimu mpya, wakati huo huo anaangalia ufiti wa mchezaji mmoja
mmoja”.
“ Baada ya wiki moja tutaanza mazoezi rasmi kwaajili ya
Kagame, mwalimu amesema michuano hiyo ni pre-season yetu ya kwanza, baada ya
Kagame tutakuwa na pre-season ya pili ambapo itabidi timu itoke kwa takribani wiki
tatu au nne kuweka kambi nje ya nchi, mipango inaendelea kujua ni wapi
tutakwenda, itakapokuwa tayari tutasema”.
“Tutarudi nchini tarehe 9 mwezi wa nane kwaajili ya mechi ya
ngao ya jamii ambapo itakuwa kati ya tarehe 15 na baada ya hapo tutaanza ligi
Agosti 22”.
0 comments:
Post a Comment