Monday, June 29, 2015

Uongozi wa Azam FC umesema, timu yao itashiriki michuano ya kombe la vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame Cup lakini maandalizi yao ni kwa ajili ya ligi kuu msimu ujao na michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho barani Afrika na hawafanyi maandalizi kwa ajili ya Kagame kama wengi wanvyodahani kwa sababu mashindano hayo hawajayapa kikaumbe ndani ya timu yao na watayatumia kama sehemu ya maandalizi yao.
Afisa mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba amesema, timu yao itashiriki mashindano hayo lakini hawayapi kipaumbele na watatumia michuano hiyo kuwachezesha vijana na wachezaji wengine wachache ambao hawakuitwa kwenye timu zao za taifa ili kutoa nafasi ya kupumzika kwa wale waliokuwa wanazitumikia timu zao za Taifa.
“Mandalizi yanaendelea vizuri timu inafanya mazoezi mara moja kwa siku na timu nzima ipo isipokuwa wachezaji ambao wapo kwenye timu zao za taifa lakini wengine wote wapo, wachezaji wengine watatu wanatarajia kuwasili siku mbili zijazo kwasababu walikuwa wameomba ruhusa walikuwa wanamatatizo ya kifamilia lakini wengine wote wapo kambini”, amesema Kawemba.
“Kuhusu Kagame kwakweli sio ‘priority’ yetu, tunaomba radhi kwa waandaaji wa mashindano hayo. Tutacheza, lakini tutashiriki kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao ambao itakuwa ni kuandaa timu yetu kwa ajili ya ‘premier league’ na confederation Cup. Kwahiyo tunaichukua Kagame kama mechi za kirafiki za kimataifa katika maandalizi yetu ya msimu unaokuja”, alieleza.
“Kwasababu kisayansi ili uweze kucheza kwenye mashindano makubwa kama hayo unatakiwa uwe umejiandaa kwa wiki kuanzia saba hadi nane uwe umefanya mazoezi, huwezi kuingia kwenye mashindano makubwa kma haya ukiwa umejiandaa kwa wiki nne. Lakinin sisi tupo kwenye kipindi cha pre season kwahiyo tunachukua mashindano haya ikiwa kama sehemu ya pre season yetu na mashindano kamili sisi tunayo jiandaa nayo ni premier league na confederation cup”, aliffanua.
“Tunatarajia kupumzisha wachezaji wetu wote ambao wako kwenye timu za taifa kwasababu watakuwa wamechoka na tutatumia wachezaji wetu wa kikosi cha pili na wachezaji wengine wachache ambao hawakuwepo kwenye vikosi vya timu zao za taifa”, alimaliza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video